Viongozi wa kidini Pwani wametakiwa kuwapa ushauri mwafaka vijana ili kujiepusha na misimamo mikali ya kidini.
Mkurugenzi wa shirika la Huria ,Yusuf Lule alisema hayo baada ya kugundulika kuwa vijana wengi wamejiunga na makundi haramu ambayo yanatekeleza uhalifu humu nchini.
Akizungumza siku ya Jumamosi huko Kilifi, Lule amewataka viongozi hao kuandaa makongamano ya amani na utangamano yatakayo wabadilisha vijana na kuanza kuwa raia wema kwa jamii.
Kauli hii inajiri baada ya kugundulika kuwa vijana wengi wamejiunga na makundi haramu ambayo yanatekeleza uhalifu humu nchini.
Lule amesema shirika la Huria linaendeleza hamasa zaidi kwa vijana hao sawia na kuhakikisha kuwa wamepata mbinu nyengine za kujipatia riziki maishani mwao.