Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Viongozi wanaotumia vijana kutekeleza uhalifu na kutia wakazi hofu wameonywa vikali, huku viongozi wa kisiasa wakitakiwa kuwataja wanaofadhili magenge ya vijana wahalifu Mombasa.

Akihutubia wananchi siku ya Jumosi katika uwanja wa Tononoka mjini Mombasa, kamishna wa Kaunti  ya Mombasa Nelson Marwa aliwataka wanasiasa wa Mombasa kuuza sera na wala sio kutumia vijana kuvurugu amani.

Marwa alieleza kwamba uchunguzi unaendelea dhidi ya jamaa mmoja aliyekuwa mfanyakazi wa serikali aliyetiwa mbaroni kwa madai ya kufundisha magenge uhalifu, huku afisa mmoja kaunti ya Lamu akishukiwa kwa madai sawa na hayo.

Wakati huo huo, Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho amewataka wakazi kujikakamua katika kupiga vita ugaidi ili usalama uimarike katika kaunti ya Mombasa.

Aidha, aliongeza kuwa ushirikiano baina ya maafisa wa usalama na raia ndio nguzo kuu ya kuboresha usalama nchini.