Vituo vya polisi ambavyo vinaendelea kujengwa na hazina ya ustawishaji maendeleo kwenye eneo bunge la Rongai (CDF), vitasaidia kupigana na wizi wa mifugo.
Akizungumza na mwandishi huyu Alhamisi Mbunge wa Rongai Raymond Moi alisema kwamba wizi wa mifugo umewahangaisha wafugaji na kurudisha nyuma kimaendeleo jamii inayotegemea mifugo.
Raymond amesema usalama ukiimarishwa utasaidia kuinua uchumi wa Rongai ambao kwa sasa uko chini mno.
Kulingana na mtunga sheria huyo, wazee wa Nyumba Kumi na machifu wanapaswa kushirikiana na idara ya polisi kuona kwamba, watu ambao wanaendelea kuwahangaisha wananchi wamekamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
CDF imejenga vituo vya polisi kwenye wadi zote tano za Rongai, na tutaendelea kuhakikisha kwamba vituo hivyo vimepata vifaa vya kutumia ili kudumisha usalama,” alisema bw Raymond Moi.