Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Huku kampeni ya kampuni ya kuuza pikipiki za Bajaj ikikamilika siku ya Jumamosi, wamiliki wa pikipiki pamoja na wahudumu wa bodaboda wameishukuru shirika hilo kwa kuwapa huduma za jinsi ya kushughulikia mitambo yao pindi inapoharibika.

Wakiongozwa na Suleiman Thoya, wahudumu hao walipata nafasi ya kujionea na kujifunza mengi kutoka kwa timu ya Shirika hilo la Boxer kwa kuelekezwa jinsi ya kutunza pikipiki zao.

Hafla hiyo ambayo iliandaliwa katika shule ya msingi ya Khadija, katika eneo bunge la Kisauni, ilishuhudia wengi wa wateja ambao walikuja kununua pikipiki, ambapo waliweza kuonyeshwa jinsi ya kutumia na kufundishwa mbinu mwafaka za kujizuia kusababisha ajali.

Hamisi Charo, ambaye pia alishiriki kwenye maenyesho hayo, alisema kuwa amekuwa barabarani kwa miaka minne akitumia aina nyingine za pikipiki, na kuahidi kununua pikipiki ya Bajaj kufuatia mafunzo na uhusiano mwema ulionyeshwa na maafisa wa shirika hilo siku ya maonyesho hayo.

“Mimi nipo tayari kununua pikipiki za Bajaj, kwa vile nimeona ni pikipiki nzuri. Maafisa wa shirika hili wanajali maslahi ya wahudumu kinyume na baadhi ya mashirika ya kutengeneza na kuuza pikipiki nchini ambao hawajali wateja wao,” alisema Charo.