Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wagonjwa wanaohitaji upasuaji kama vile upasuaji wa vibofu vya mkojo katika Kaunti Mombasa watafaidika na matibabu ya opareshini kwa malipo ya chini.

Akizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumanne katika Hospitali ya Sayyida Fatima, iliyoko katika Kaunti ya Mombasa, Dr Aboubakar Badawi, alisema kuwa wanaougua magonjwa ya kizazi wataweza kufaidika na oparesheni kwa malipo ya chini, kufuatia muungano wa madaktari wa 'Doctors Without Borders' kutoa vifaa na dawa zilizogharimu shilingi milioni 500,000.

Aidha, Dkt Badawi alisema kuwa madaktari katika Hospitali ya Sayyida Fatima watapewa mafunzo kutibu magonjwa mbali mbali yanayohitaji upasuaji ili wakazi wapate afya bora kwa malipo ya chini.

Kulingana na daktari huyo, wagonjwa 41 kutoka Kaunti za Mombasa na Kilifi waliokuwa walipe shilingi laki mbili na nusu walipata matibabu hayo bure baada ya madaktari hao kufadhili gharama za matibabu hayo.

Aidha, Dkt Ihsan Karaman alisema kuwa wagonjwa mbali mbali wanaohitaji upasuaji wamejitokeza katika msukumo wa muungano huo, huku akitaka wakazi wanaougua kujitokeza ili wapate matibabu hayo.