Huku kura zikiwa zimepigwa vijana wengi wamekosekana kwenye upigaji kura wa eneo la Malindi ambapo kulingana na utafiti wa makala haya umeweza kubainisha kuwa kina mama pamoja na raia wenye umri mkubwa au wazazi ndio walionekana wakijihusisha kwenye upigaji kura na
Wakaazi katika eneo la Pwani wametoa ombi kwa Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kubadilisha siku za upigaji kura kuwa za wikendi pekee, ili iwe rahisi kwa wale wanaoenda kazini kushiriki katika zoezi hilo.
Baadhi ya wenyeji ambao waliongea na mwandishi huyu katika baadhi ya vituo vya upigaji kura walisema kuwa wengi wa wapiga kura huja wakiwa wamechelewa kwa kuwa wao hulazimika kuenda kazini kwanza.
Fatuma Chiro, ambaye ni mkaazi wa Mombasa na mzaliwa wa Malindi, alitoa lawama kwa Tume ya IEBC pamoja na serikali kwa kukosa kuzingatia kuwa wakaazi huenda kazini, hatua aliyosema mara nyingi huwafungia wengine kushiriki haki yao ya kupiga kura.
“Serikali sharti ikome kuendelea kutumia siku za wiki kufanya shughuli muhimu kama hizi za kupiga kura, ambapo huwa vigumu kwa wengine wetu ambao tunafanya kazi kushiriki zoezi hizo. Wanataka watu waache kazi zao na kuenda kupiga kura alafu baadaye wafutwe kazi ilhali kazi hazipatikani siku hizi,” alisema Chiro.
Salim Guyo, ambaye ni mmoja wa wanasiasa wanao azma ya kuwania kiti cha uwakilishi Wadi ya Ganjani, Kaunti ya Mombasa, aliunga mkono kauli hiyo na kusema kuwa kura huwa muhimu na sharti siku za kupiga kura ziwe wikendi ndio kuwapatia wananchi nafasi ya kushiriki katika uchaguzi kikamilifu.