Samson Otieno mkaazi katika kijiji cha Darajani, Kibera amewaomba na kuwasihi wakaazi wenzake kutokubali hongo kutoka viongozi ili kubadilisha kituo cha kupigia kura.
Kulingana na Otieno, kila mkaazi yuko na uhuru wa kujisajili kama mpiga kura katika kituo chochote anachohitaji kando na kuhongwa na wanasiasa au viongozi wanaotaka kupigiwa kura.
Otieno aliyekuwa akizungumza leo asubuhi alisema kuwa kuna baadhi ya viongozi ambao wameanza kudanganya wakaazi wengine kuchukua kura katika vituo tofauti ili kupata afueni ya kupata uungwaji mkono katika uchaguzi ujao.
“Hakuna kiongozi yeyote ambaye anaruhusiwa kuwadanganya wananchi kushika kura katika vituo tofauti. Kama ni kujisajili, jisajili katika eneo upendayo,’’ alisema Otieno.
Otieno alidai kuwa kuna baadhi ya fununu kutoka sehemu jirani kama Kawangware, Kangemi, Uthiru na Dagoretti kuwa inashukiwa kwamba baadhi ya viongozi kutoka sehemu hizi wameanza mikakati ya kuhonga wakaazi wa Kibera ili kujisajili kwenye eneo hizi ili wapate kuungwa mkono ifikapo mwaka wa 2017.
‘‘Ikiwa mkaazi anahitaji kubadilisha uongozi mbaya katika eneo lake ni lazima ajiandikishe kama mpiga kura katika eneo lake na asikubali hongo na kutumiwa vibaya na viongozi walio na tama,’’ alisema Otieno.