Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakaazi wa mitaa ya Flamingo, Pangani na Lakeview viungani mwa mji wa Nakuru wameshauriwa kushirikiana na vyombo vya kiusalama na kuripoti visa vyovyote vinavyonuia kutatiza usalama wao.

Haya ni kufuatia madai ya kuzuka kwa hofu ambayo imeenea kwa siku mbili sasa kuhusu makundi haramu ikiwemo Mungiki yanayodaiwa kuwa na lengo la kutatiza usalama katika maeneo hayo.

Wito huo umetolewa na aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha TNA tawi la Nakuru Dkt Abdul Nooor.

Noor alisema kuwa wengi wa wakaazi wameripoti kuwa wanaishi kwa hofu baada ya makundi hayo ambayo lengo lake haswa halijabainika, kudaiwa kufurika eneo hilo.

Kulingana na wakaazi waliohojiwa Alhamisi , makundi hayo awali yalitishia kufanya uhalifu lakini wenyeji wa maeneo hayo wakapuuza madai hayo, kisha baadaye makundi hayo yakavamia siku chache.

Hata hivyo Noor alidokeza kuwa kupitia kwa ushirikiano na maafisa wa usalama chini ya OCPD wa Nakuru Musa Kongoli, hali hiyo imethibitiwa huku akiwataka wananchi kukaa kwa amani.

"Haiwezekani watu katika taifa lao kuishi kwa hofu ya kushambuliwa na wachache ambao wanajitakia mambo ya kibinafsi. Wananchi washirikiane na polisi,"Abdul Noor alisema.