Baadhi ya wakazi Nyamira wameunga mkono juhudi na mikakati aliyoweka kamishna wa kaunti Josphine Onunga kupambana na ukosefu wa usalama.
Wakihutubu katika eneo la Enchoro siku ya jumanne, wakazi hao wakiongozwa na msemaji wao Peter Nyakeri walisema kuwa kujitolea kwake kamishna Onunga kumesaidia pakubwa kudhibiti visa vya ukosefu wa usalama katika maeneo mengi Nyamira.
"Kwa kweli sisi wakazi wa Enchoro tumefurahishwa sana na mbinu anazozitumia kamishna Onunga kuimarisha usalama kote Nyamira na hatua yake yakuwahuzisha machifu, manaibu wao pamoja na wananchi wa kawaida umesaidia pakubwa kupunguza visa vya utovu wa usalama,” alisema Nyakeri.
Wakazi hao aidha walisema kuwa juhudi zake Onunga zimesaidia kubadilisha tabia za vijana ambao wamekuwa wakijihuzisha na visa vya uhalifu ambao kwa sasa wameasi tabia hiyo nakuanzisha miradi yakuwastawisha kimaendeleo.
"Tangu kamishna Onunga aanzishe mikakati yakuimarisha usalama kwa kweli idadi kubwa ya vijana ambao wamekuwa wakijihuzisha na visa vya uhalifu wameasi kabisa tabia hiyo nakuanza kutekeleza miradi muhimu kama ya ufugaji kuku swala ambalo nilakufurahisha sana," aliongezea Nyakeri.