Wananchi katika Kaunti ya Nakuru wameelezea furaha yao baada ya bei ya mafuta taa kupungua kwa Sh1.54 kwa lita.
Kulingana na bei mpya zilizotolewa Jumatatu na tume ya kudhibiti kawi nchini ERC, bei ya chini zaidi itakuwa mjini Mombasa ambapo lita moja ya mafuta hayo itauzwa kwa Sh50.55, huku ya juu zaidi ikiwa Sh57.23 huko Isbania.
“Wakati huu wa sherehe ni vyema bei za bidhaa ziwe chini, na tangazo kama hilo bila shaka ni la kupongezwa,” alisema Nelson Mwangi, mkazi.
Bei hizo mpya zitatumika kuanzia hii leo, Jumanne Desemba 15 hadi Januari 14 mwaka 2016.
Madereva watatabasamu pia kwani bei ya petroli imepungua kwa Sh0.40, huku Diseli ikishuka kwa Sh1.15.
Kwa ujumla bei ya chini zaidi ya petroli itakuwa Sh86.75, huku ya juu zaidi ikiwa Sh94.10. Dizeli itauzwa kwa kati ya Sh75.23 na Sh82.73.
Dereva mmoja kwa jina John Mwangi wa magari yanayobeba abiria kutoka mjini Nakuru kwenda Subukia, alisema sasa itakuwa vigumu kwa wenye matatu kuwaamuru kuongeza abiria nauli, ikizingatiwa bei ya chini ya mafuta