Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Idara ya usalama mjini Mombasa imewataka wananchi kutokuwa na hofu watakaposikia milio ya risasi pamoja na mizinga ikitokea eneo la Mtongwe ama baharii upande wa Likoni.

Hili ni kutokana na kuendelea kwa mazoezi ya kivita ya wanajeshi wa wanamaji katika kambi yao ya Likoni huko Mtongwe.

Mwenyekiti wa kamati ya usalama Nelson Marwa ametoa wito kwa wakazi wanaoishi karibu na maeneo ya kambi hiyo kama vile Mwangala, Dongo Kundu na maeneo mingine yanayopakana na kambi hiyo kutokuwa na hofu pindi watakaposikia milio hiyo.

Akizungumza na mwanahabari huyu siku ya Jumatano, Marwa alisema hali ya usalama iko shwari na hakuna tishio lolote la kiusalama, hivyo basi wananchi kutofikiri kuwa milio hiyo inatokana na uvamizi wa kundi la kigaidi la Al shabaab.

Alisema zoezi hilo huenda likadumu kwa takriban juma moja.