Wakazi wa kaunti ya Nyamira wameombwa kutochukua sheria mikononi mwao wanapomfumania mshukiwa wa wizi ila kuripoti kwa kituo cha polisi.
Ombi hilo lilitolewa baada ya wakazi wa eneo la Nyabite kaunti ya Nyamira kumfumania mshukiwa wa wizi na kuanza kumshambulia vikali lakini kwa bahati nzuri akaokolewa na maafisa wa polisi.
Akizungumza siku ya Jumatatu mkuu wa polisi mjini Nyamira Ricah Ongare alisema hakuna sheria inaruhusu mwananchi yeyote kumshambulia mwezake ila kuripoti kwa kituo cha polisi.
“Naomba kila mkazi anapomfumania mshukiwa wa wizi aripoti kwa kituo cha polisi kilicho karibu badala ya kushambulia mshukiwa ,” alisema Ricah Ongare.
Wakazi wakishuhudia mshukiwa wa wizi akishambuliwa.wakazi hao wameombwa kutochukua sheria mikononi mwao wanapomfumania mshukiwa wa wizi i[Dennis N/hivisasa.com]