Share news tips with us here at Hivisasa

Watu ambao wamekuwa na uzoefu wa kuzuru maeneo ya shule wakati shule zimefungwa wameonywa vikali dhidi ya kusababisha uharibifu katika shule hizo

Akizungumza na mwandishi huyu wa habari siku ya Alhamisi mjini Marani,  mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi ya Nyakeiri Stevin Morara alitoa ilani kwa wakazi ambao wanapenda kuenda katika maeneo ya shule nyakati za likizo ili kubarizi.

Kulingana na mwalimu huyo, wanaotabia za kuzuru shuleni nyakati za likizo watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwa watafumaniwa kwani hawana la kufanya shuleni humo.

“Watu hawa wanapozuru mashule wanasababisha madhara mengi yenye gharama za juu kwenye shule, na hilo hatutalikubali kuendelea, maana hilo si jambo nzuri,” alisema Morara.

“Mara nyingi wakati wa likizo tunashtukia vifaa vya shule vinapotea huku mali nyingi ikiharibiwa haswa madirisha na mengine mengi, natoa onyo yeyote akipatikana atachukuliwa hatua kali za kisheria,” aliongezea Morara.

Aidha, wakazi walio karibu na mashule walisema hapo awali kuwa baadhi ya watu hulisha mifugo wao shuleni huku wakishukiwa kufanya hilo.