Naibu wa Rais William Ruto amewahimiza wananchi kushirikiana pamoja katika kuendeleza maendeleo nchini na kusahau tofauti zao.
"Tushirikiane kwa umoja kama wakenya, sisi zote tujuwe nimapenzi ya mungu vile tulivyo, ukabila italemaza maendeleo ya nchi," alisema Ruto.
Ruto pia amewaomba wakenya kujali hali ya kila mmoja kama njia mojawapo ya kuleta amani, uwiano na kuboresha hali ya usalama nchini.
“Mimi nawasihi tuweke undugu, tuweke umoja na tushirikiane kwa mapenzi, wenye mali wenye hawana tupendane na tukae pamoja ili kujenga nchi yetu” aliogeza Ruto.
Ruto alikuwa akizungumza katika eneo la Kapsaret, Kaunti ya Uasin Gishu alikofungua makanisa matatu yakiwemo kanisa la Angikana ya Lemook , Mosobor AIC pamoja na kanisa la kikatoliki kwa jina St Pauls.