Walinzi 15 wa Kampuni ya ulinzi ya kibinafsi ya Solvit walifikishwa mahakani siku ya Jumanne kwa madai ya kuzua vugurugu na kutishia kumpiga raia wa China.
Mahakama ilielezwa kuwa mnamo tarehe Novemba 1, 2015, walinzi hao wanadaiwa kumtishia Artist Lexao, ambaye ni raia wa China, kwa kumpiga kwa marungu katika Kampuni ya gesi ya Agoli iliyoko eneo la Miritini.
Walinzi hao walikanusha madai hayo mbele ya Hakimu Mkuu wa Mombasa, Susan Shitub.
Hakimu Shitub aliwaachilia walinzi hao kwa dhamana ya Sh10,000 ama Sh3,000 pesa taslimu.
Kesi hiyo itasikizwa Disemba 10, 2015.