Wafanyibiashara wa jua kali katika eneo la Nyabite mjini Nyamira wameomba serikali ya kaunti ya Nyamira kuwajengea vibanda ili kutosumbuliwa na mvua ambayo imeanza kunyesha katika eneo hilo.
Wito huo umetolewa baada ya wafanyibiashara hao kupata wakati mgumu kufanya kazi yao siku nzima haswa mvua inapoanza kunyesha.
Wakizungumza nasi siku ya Jumatano katika eneo hilo la Nyabite, wafanyibiashara hao wa juakali wakiongozwa na mtengenezaji wa magari Jadson Nyaribo, walisema biashara zao hutatizwa pindi mvua inapokunya na kulazimika kufunga biashara zao kwani hawana pa kujikinga.
Kulingana nao, wao hutoa ushuru kwa serikali ya kaunti hiyo na wameomba kaunti hiyo kutumia pesa hizo kuwajali na kuwajengea vibanda hivyo ili sekta yao ya biashara iweze kuinuka zaidi.
“Sisi wana juakali tunapata muda mgumu zaidi mvua ikinyesha maana tunafunga biashara zutu kwa kukosa pa kujikinga," alisema Nyaribo.
tunaomba serikali kutujengea vibanda ili tuwe tunafanya kazi zetu hadi siku kukamilika bila kufunga kwa kuhofia hali ya anga,” alieleza Nyaribo.