Mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri amewaomba wanafunzi wa darasa la nane wanaosubiri matokeo ya mtihani wao hii leo, kutokata tamaa maishani.
Akizungumza na baadhi ya wanafunzi hao jumanne, Ngunjiri alisema kuwa kuna haja ya wale watakaofeli mtihani kujiunga na vyuo vya anuwai ili kujifunza mafunzo tofauti.
"Ningewaomba nyinyi vijana kujiepusha na mihadarati kwani kuanguka mtihani sio mwisho wa mafanikio, kuna shule ambazo mnaweza kujiunga na kupata mafunzo kama vile ufundi, uendeshaji magari, mijengo akiwemo zingine," alisema Ngunjiri.
Haya yanajiri siku chache baada ya ofisi ya CDF ya Bahati kuwakabidhi zaidi ya vijana mia mbili hati ya uendeshaji magari huku mbunge huyo akiahidi kuwajumuisha vijana ambao watakosa nafasi katika shule za upili.