Share news tips with us here at Hivisasa

Wanasiasa mbalimbali wa mrengo wa Cord wanaendelea kuikashifu hatua ya polisi ya kuondoa maafisa wa ulinzi wa gavana wa kaunti ya Mombasa Hassan Joho.

Viongozi hao wanasema kwamba hatua hiyo ni njama ya serikali ya kukandamiza muungano wa Cord eneo la Pwani baada ya kuona muungano huo unaendelea kuimarika eneo hilo.

Mbunge wa Mvita Abdulswamad Sharif Nasir anasema kuwa maafisa wa ulinzi wa gavana walikamatwa kutokana na ushindi wa Cord katika eneo bunge la Malindi uliofanyika hivi majuzi.

Mwingine aliyejitokeza na kupinga hatua hiyo ni mbunge wa Gem Jakoyo Midiwo aliyetaja tukio hilo kama kinyume cha sheria, akiongeza kuwa Gavana Joho ana haki ya kupata ulinzi kwa mujibu wa sheria.

Mapema siku ya Alhamisi ilidaiwa kwamba idara ya polisi iliwaondoa kazini maafisa saba wa usalama waliokuwa wakimlinda Gavana Joho huku ikisemekana kwamba wameenda masomoni.

Picha: Mbunge wa Mvita Abdulswamad Nasir. Nasir anasema kuwa anapinga kuondolewa kwa walinzi wa Joho akisisitiza kwamba ni kinyume cha sheria. Maktaba