Share news tips with us here at Hivisasa

Mwakilishi wa wanawake katika Kaunti ya Nakuru Bi Mary Mbugua amepongeza chama cha Maendeleo ya Wanawake kwa kusimama kidete na mwenyekiti wao wa tawi la Nakuru Bi Keziah Ngina, alijeruhiwa katika ajali ya barabarani.

Akizungumza siku ya Jumamosi wakati wa hafla ya kuchangisha fedha za kugharamia matibabu ya Ngina, Bi Mbugua alisema kuwa ni jambo la busara kwa wanawake kushirikiana katika jamii.

"Mimi nataka kuwapongeza sana akina mama wanachama wa Maendeleo ya Wanawake kwa kusima na mwenzetu Ngina,” alisema Mbugua.

Wakati huo huo, Mbugua alitoa wito kwa akina mama na vijana kujiandikisha katika vikundi ili kunufaika na fedha walizotengewa na serikali.

"Ningepeenda kuwaambia kwamba kuna fedha zimetengwa na serikali na ni wajibu wenu kujiunga katika makundi ili mnufaike na fedha hizo," alisema Mbugua.

Naibu Rais Wiliam Ruto alituma mchango wake wa shilingi 500,000.