Washukiwa wa ulanguzi wa Pembe za wanyama-pori walioshtakiwa hapa Mombasa, sasa wanatuhumiwa kufadhili kwa ugaidi na ulanguzi wa mihadarati kaunti hii.
Washukiwa hao, Ali Omar Haji na Said Alfani Mwinyi wanadaiwa kupatikana na pembe za kifaru zenye thamani ya shilingi milioni 3.
Polisi wameiambia mahakama kupitia wakili wa serikali Jami Yamina, kuwa madai mapya yaliochipuka ni kutokana na uchunguzi wa awali uliofanyiwa simu zao za mkononi.
Hata hivyo, Yamina ameomba muda zaidi kuwasilisha ushahidi zaidi japo mawakili wa washukiwa wakiongozwa na Pascal Nabwana wamepinga madai hayo wakidai kuwa mahakama inawakandamiza wateja wao.
Mawakili hao waliomba serikali iwaachilie wateja wao kwa dhamana.
Upande wa mashtaka unatarajiwa kuwasilisha nakala nyengine ya ushahidi kuhusiana na kesi hiyo.