Wanawake watatu na mwanamume mmoja wamefikishwa katika mahakama kuu ya Mombasa na kufunguliwa mashtaka ya mauaji.
Upande wa mashtaka ulielezea mahakama siku ya Jumatatu kuwa washukiwa hao, Kwekwe Luganje, Mwaka Luganje, Machemunda Mboga, na Masha Wanje Mwadori wanadaiwa kumuua Luganje Mwandori mnamo Novemba 28, 2015, katika mtaa wa Nzombo huko Kinango, Kaunti ya Kwale.
Wanne hao walikana mashtaka hayo mbele ya Jaji Asenath Ongeri.
Washukiwa hao watasalia rumande hadi tarehe Machi 14, 2016.