Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Maafisa wa polisi eneo la Kisauni wamewapiga risasi vijana wawili wanaoshukiwa kuwa wa kundi haramu la “wakali Kwanza” wanaoaminika kuwahangaisha wakazi.

Aktithibitisha kisa hicho siku ya Jumamosi, naibu kamishana wa Mombasa Julius Kavita alisema uchunguzi kuhusiana na kisa hicho unaendelea.

Aidha, aliongeza kuwa idara ya usalama iko imara katika kuangamiza kundi hilo haramu linalowasumbua wananchi.

Kavita alisitiza kuwa vijana hao walikuwa wamejihami kwa silaha hatari kama vile panga na visu huku wakiwa na nia ya kutekeleza wizi na uahalifu miongoni mwa jamii nyakati za usiku.

Maeneo ya Kisauni yamekuwa yakikumbwa na visa vya uhalifu unaotekelezwa na vijana wadogo huku idara ya polisi kaunti ya Mombasa ikiahidi kumaliza magenge yote ya uhalifu.