Wasiwasi umeanza kushuhudiwa katika mtaa wa Likoni baada ya taarifa za kuzuka kwa maradhi ya kipindupindu kusaamba eneo hilo huku wakaazi wakiombwa kuchukua taathari.
Hospitali ya Mrima eneo hilo ilitangaza kupokea wagonjwa siku siku ya Alhamisi wanaoaminika kuathiriwa na maradhi hayo.
Ingawaje kisa hicho kilihusishwa na familia moja sehemu hiyo, mafisa wa afya eneo hilo wanaendelea na uchunguzi kubaini iwapo kuna mkurupuko wa maradhi hayo hatari.
Visa hivyo vinaripotiwa huku ikiaminika kwamba baadhi ya mitaa eneo hilo la Likoni ni duni, huku wengi wa wakaazi wakiishi katika hali ya umaskini.
Baadhi ya wakazi hawana vyoo, na maafisa wa usalama wamewahimiza wakazi kuchimba vyoo baada ya kubainika kwamba wengi wao hawana vifaa hivyo muhimu.
Hospitali ndogo ya Mrima imeweka hema maalum hospitalini humo ili kuwashughulikia wagonjwa watakaoonyesha kuwa na dalili za maradhi hayo.