Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Watu watano walifariki katika ajali iliyofanyika usiku wa kuamkia Ijumaa, karibu na chuo cha mafunzo ya ualimu cha NTTC kilomita tatu kutoka kituo cha kibiashara cha Salgaa barabara ya Nakuru-Eldoret.

Ajali hiyo ilifanyika wakati gari ndogo aina ya Toyota lililokuwa likitoka Nakuru baada ya kupoteza mwelekeo na kuingia chini ya basi moja.

Akidhibitisha ajali hio,  kamanda wa trafiki eneo la Salgaa Walter Kiptala alisema: “Abiria waliokuwa kwenye basi hawakupata majeraha yoyote. Watano waliofariki ni waliokuwa kwenye gari hilo."

Alisema miili ya marehemu ilipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti mjini Nakuru.

Ajali hiyo ilisababisha msongamano mkubwa wa magari kwenye barabara hiyo.

Kiptala alitoa onyo kwa madereva wa magari ya kibinafsi kuwa watakamatwa wakipatikana kukiuka sheria za trafiki, ama kubeba abiria kinyume cha sheria.