Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wazazi kutoka Kaunti ya Kisii wameiomba serikali kuwapunguzia bei ya vitabu vya kusoma, ambayo walisema imepanda katika siku za hivi maajuzi.

Wakizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatatu mjini Kisii, wazazi hao, wakiongozwa na Mary Kerubo, waliomba serikali kuwapa msaada kwa kupunguza bei ya vitabu vya kusoma kwa kuwa gharama ya maisha pia imepanda.

Wazazi hao waliitaka serikali kuweka mikakati kapambe kuhakikisha kuwa bei hiyo imepunguzwa.

“Bei ya vitabu kwa sasa imeonekana kuongezeka zaidi. Tunaomba seikali itupunguzie mzigo huo kwani pia gharama ya maisha imepanda, na hatuna mahala pa kukimbilia,” alisema Kerubo.

Bei ya vitabu katika siku za hivi maajuzi iliongezwa kwa kile kilichotajwa kama ongezeko la bei ya makaratasi ya kutengeneza vitabu hivyo, ambavyo husafirishwa kutoka nje ya nchi.

Wazazi hao walisema kuwa baadhi ya vitabu vilivyopandishwa bei ni vitabu vya hesabati, kamusi ya kingereza na ile ya Kiswahili, kitabu cha Kiswahili Lugha, miongoni mwa vitabu vingine.