Share news tips with us here at Hivisasa

Mwalimu wa shule ya upili ya wasichana ya Sironga kaunti ya Nyamira Hellen Mabese ametangaza wazi kwamba zaidi ya wanafunzi 250 walioketimtihani wa kitaifa wa kidato cha nne mwaka jana watajiunga na vyuo vikuu. 

Akihutubia wanahabari shuleni humo baada ya waziri wa elimu nchini Fred Matiang'i kutangaza wazi matokeo ya mtihani huo mapema alhamisi, Mabese alisema kuwa shule hiyo ilifanikiwa kurekodi matokea ya alama wastani ya 9.7, inavyolinganishwa na alama wastani ya 8.90 mwaka jana. 

"Kwa hakika nimefurahi sana kwa maana shule hii inaendelea kutia fora hata zaidi kwa maana tumefanikiwa kurekodi alama wastani ya 9.7 kwenye matokeo ya mtihani huu na zaidi ya wanafunzi mia 250 walioketi kuufanya mtihani wa mwaka jana watafanikiwa kujiunga na vyuo vikuu na natumai tutafanya vyema zaidi mwaka huu," alisema Mabese. 

Mabese aidha aliongeza kusema kuwa matokeo mazuri ya mwaka huu yalitokana na ushirikiano wa karibu kati ya wanafunzi na walimu, hali aliyosema imekuwa nguzo muhimu shuleni humo. 

"Kwa shule kufanikiwa kupata alama 45 zikiwa A, hiyo ni ishara wazi kwamba wanafunzi wetu walitia bidii masomoni na kwa hakika tulikuwa na matarajio kuwa wangefanya vyema ila haya tu yamewezekana kwa sababu ya ushirikiano mzuri kati ya walimu na wanafunzi," aliongezea Mabese.