Wito umetolewa kwa wahudumu wa tuktuk na bodaboda katika kaunti ya Mombasa kuzingatia sheria za trafiki barabarani ili kuzuia kushughudiwa kwa ajali.
Mwenyekiti wa Chama cha Wahudumu wa Tuktuk katika kaunti ya Mombasa Obedi Miruli amewataka madereva wa tuktuk na bodaboda kuwa waangalifu sambamba na kuzingitia sheria za trafiki.
Akizungumza mjini Mombasa siku ya Jumanne, Bw Miruli alisema kuwa abiria wengi wamekuwa wakilalamikia huduma duni kutoka kwa wahudumu hao na akawataka kuwaheshimu wateja wao ili kuboreshwa kwa sekta hiyo ya uchukuzi.
Alisema kuwa visa vya ajali za barabarani vitasitishwa kwa kiwango kikubwa iwapo madereva wa tuktuk, bodaboda, magari ya uchukuzi wa umma na abiria watazingatia sheria za trafiki.
"Tunawatahadhari wahudumu wa tuktuk na badobado kuzingitia sheira za trafiki ili kuepukana na ajali za mara kwa mara barabarani kwa ajili ya usalama ya abiria," alisema Miruli.
Hata hivyo alisema kuwa zaidi ya tuktuk nne huhusika katika ajali ya barabarani kila mwezi.