Wamiliki wa magari katika mji wa Kisii wamewashtumu baadhi ya makanika kwa kuwatapeli pesa kwa kuwadanganya kuwa wao ni makanika wanaojua kazi kwa ustadi ilhali ni makanika ghushi.
Wakiongea na Mwadishi huyu siku ya Jumanne, baadhi ya wamiliki wa magari haswa ya kibnafsi na wanaofanya kazi ya taxi katika mji wa Kisii na Viunga vyake wamewalaumu wanaojifanya kuwa makanika wa kuwatengenezea gari ihali wao ni matapeli wala si makanika wanaoaminika kwa kazi yao ya kutengeneza magari.
“Nilishangazwa sana wakati nilipeleka gari langu kwenye gereji moja hapa Kisii ili liweze kutengenezwa na jamaa niliyepatia kunitengenezea gari ambalo halikumaliza siku tatu kabla ya kuaribika tena," alihoji Edward Oyaro mmiliki wa gari.
Aidha, Oyaro alisema kuwa vijana wengi wamejitokeza katika sekta hiyo wakiwa na ujanja kwa kuwa na tamaa ya pesa bila kujali kazi wanayofanyia wateja wao.
Kwa sasa wamewomba vijana hao kuwa waaminifu katika kazi yao na kutumia masomo waliyopata kutoka taasisi mbali mbali ili kuwa na wateja wengi wanaowaamini.
“Kuna makanika mmoja alikuwa akitengeneza magurudumu ya gari langu, lakini wakati nilitoka kuelekea Nyamira, gurudumu moja lilichomoka na ni Mungu Aliyenisaidia. Nawasihi vijana hawa kukoma kuchanganya mcheza na kazi yao maanake hiyo ni kuhatarisha maisha ya watu,” alisema Yapesh Marocha, mmiliki mwingine wa gari Kisii.
Kwingineko wamewaomba wenye magareji kuwachunguze vyema vijana wanaowaajiri kubaini kama kwa ukweli wana ujuzi huo wa kutengeneza magari kabla ya kuwapa nafsi ya kufanya kazi katika gareji hizo.