Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mwenyekiti wa Hospitali ya Nyamira Level Five Cyrus Ayunga amedai kuwa maafisa wa afya katika hospitali hiyo wanaendelea kuishi kwa uoga baada ya kutishiwa maisha yao na baadhi ya Wawakilishi wa Wadi ya Kaunti ya Nyamira.

Akizungumza na Waandishi wa habari mnamo siku ya Jumatano katika ofisi yake ilioko katika hospiatali hiyo ya Nyamira, mwenyekiti Ayunga alisema kuwa baadhi ya Wawakilishi wa Wadi katika Kaunti ya Nyamira wamekuwa wakienda moja kwa moja hadi hospitali hiyo na kuwatishia maafisa hao kuwa hawafanyi kazi yao inavyostahiliwa na hata kuwatishia misha yao.

"Kuna baadhi ya Wawakilishi wa Wadi wanao dhania kazi ambayo hutekelezwa na madaktari wa hospitali hii sio nzuri na kuwatishia na hata kutaka kuwagombanisha. Tabia hiyo sio nzuri kamwe maana hawa madaktari walisomea kazi yao na wanaijua jinsi ya kuifanya,” alihoji Ayunga.

Mwenyekiti hoyo aliongeza, “Wengi wa maafisa wa afya hapa Nyamira sasa wana uoga na hawawezi kufanya kazi yao vizuri kufuatia vitisho kutoka kwa baadhi ya Wawakilishi katika kaunti hii.”

Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, siku ya Jumamosi Mwakilishi mmoja alienda hadi hospitali hiyo na kutishia daktari aliyekuwa akihudumia mgonjwa ambaye alihusika katika ajali ya barabara ambaye walitaka ashughulikiwe kisha atumwe katika hospitali ya Tenuek kwa matibabu zaidi.

"Kufikia sasa tumeandikisha ripoti kwa Kituo cha Polisi dhidi ya Mwakilishi huyo na tunahitaji achukuliwe hatua ya kisheria," alidokeza Ayunga.

Ombi limetolewa kwa Wawakilishi wa Wadi kuheshimu madaktari na maafisa wa afya ili wafanye kazi yao jinsi wanavyoijua

"Ndio tunajua kuwa kuna baadhi ya madaktari ambao hawafanyi kazi ipasavyo, lakini kumtishia maisha sio suluhisho kuja kwa msaidizi wangu piga ripoti au uje kwangu mwenyewe na uniambie, alisema Ayunga.