Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mbunge wa Bomachoge Chache, Kaunti ya Kisii Simon Ogari ameanzisha ujenzi wa kiwanda cha kutengenenza bidhaa mbalimbali.

Bidhaa hizo ni; sabuni, maji safi ya kunywa, viatu miongoni mwa bidhaa zingine zinazotarajiwa kusaidia kuinua uchumi wa eneo hilo.

Akiongea siku ya Jumatatu katika eneo hilo la Biyonge, Mbunge Ogari alisema ujenzi huo unatekelezwa kupitia pesa za hazina ya ustawi ya maeneo bunge al maarufu CDF kwa ushirikiano na serikali kuu ili kiwanda hicho kiwasaidie wakazi wa eneo hilo na kaunti nzima ya Kisii kibiashara na kiuchumi.

“Tayari tuna mashine mbali mbali ambazo tulikabidhiwa na serikali ya kitaifa ya kutengeneza bidhaa hizo ambazo tumeandaa kutengenezwa katika kiwanda hichi,” alisema Ogari.

Ujenzi huo ulianzishwa rasmi siku ya Jumatatu na mbunge huyo wakazi wa eneo hilo wakifurahia mradi huo mpya.

Wakati uo huo, Mbunge Ogari alisema vikundi mbali mbali vitaundwa katika kiwanda hicho ili wale watakaofanya kazi kwa kiwanda hicho wajiunge kwa vikundi  hivyo na kuweka pesa zao katika Saccombali mbali ambazo zitawasaidia nyakati zijazo na kujiendeleza kimaisha.

“Tunampongeza mbunge wetu maana sasa tutakuwa tukifanya biashara kwa hali ya juu na vijana wetu watapata ajira katika kiwanda hicho,” alisema Beatrice Oiko, mkazi wa eneo hilo.