Share news tips with us here at Hivisasa

Profesa John Akama wa Chuo Kikuu cha Kisii John Akama amewaomba viongozi kutoingiza siasa kwenye mradi wa E-waste ulianzishwa Jumanne katika Kaunti ya Kisii.

Akizungumza siku ya Jumanne katika mkahawa moja mjini Kisii wakati mradi huo ulizinduliwa rasmi, Profesa Akama aliwaomba viongozi na wanasiasa kutoingiza siasa kwenye mradi huo wa maendeleo.

“Mradi huu ambao tumeanzisha wa kukusanya bidhaa hivi vya vyuma ambavyo havifanyi kazi nyumbani mwetu vimepata kazi na kuwezesha wakazi kupata pesa,” alihoji Profesa Akama.

Profesa Akama aliongeza, “Nawomba wanasisasa wote kutoleta siasa katika kila mradi, bali tuendelee mbele maana hayo yatarudisha nyuma maendeleo katika Kaunti yetu ya Kisii.”

Mradi huo wa E-waste utakusanya bidhaa vya vyuma, simu ambazo hazifanyi tena, redio na televisheni ambazo zimeharibika na kutumiwa kutengeneza bidhaa badala ya kuzitupa.

Mradi huo ni wa kwanza kuanzishwa katika Kaunti ya Kisii na ni wa kwanza kuanzishwa kwa mataifa ya Africa Mashariki.

“Haya ndio maendeleo tunahitaji katika kaunti yetu na inasemekana kuwa bidhaa hivi ambavyo tunavikusanya inasemekana kuwa vina uwezo wa kuleta magonjwa kama saratani kwa watu ndio maana serikali ya Kaunti ya Kisii kwa ushirikiano na Chuo cha Kisii kiliona ni heri mradi huo uanzishwa katika kaunti hiyo ili maisha ya watu yasiwe hatarini,” alisistiza Profesa Akama.