Share news tips with us here at Hivisasa

Mwakilishi wa wadi ya Kiplombe, Ramathan Ali, ameushutumu uongozi wa kampuni ya Raiply kwa kukosa kujitayarisha kikamilifu kwa mikasa.

Akizungumza siku ya Jumatano wakati wa mkasa huo wa moto, Ali alisema kuwa kampuni hiyo ingefaa kuweka mikakati madhubuti ya kukabiliana na majanga ya moto.

Ali aidha alisema kuwa wanamatumaini wa kuuzima moto huo ambao unasambazwa kwa haraka kwa ajili ya upepo.

"Timu za kukabiliana na mikasa ziko hapa kudhibiti janga hili na tuna matumaini kuwa wataweza kudhibiti moto huu,” alisema Ali.

Mwakilishi huyo aliiomba serikali kuu kusaidia kaunti mbalimbali kupata ndege itakayo saidi kukabiliana na majanga kama hayo.

Moto huo ulikuwa tayari umeanza kuvuka hadi kwenye stoo ya mabaki ya mbao ilioko upande mwingine.