Wakazi wa Gesima Kaunti ya Nyamira wameiomba serikali kuwapatia jukumu la kuwachagua chifu na naibu wake.
Wamesema ni vyema wajichagulie viongozi hao wenyewe kwani watamfahamu mtu ambaye atafanya kazi katika lokesheni yao kwa njia ya uwazi.
Wakiongea siku ya Jumapili Katika soko la Gesima eneo bunge la Kitutu Masaba mwenyekiti wa kikundi cha wakulima cha eneo hilo Zablon Mocheche alisema wanastahili kumchagua chifu na manaibu wake ili kuondoa mapendeleo.
Aidha, walisema wakuu hao wa lokesheni hawawajibiki kazini wamidai viongozi hao hudai wanawajibikia serikali na sio wakazi amabao hawakuwachagua.
“Tunaomba tupewe jukumu la kumchagua chifu na naibu wake kwa kuwa sisi kama wananchi ndio tunawafahamu wale watakaofanya kazi kwa ukamilifu,” Mocheche alisema.
Pia, wamewaomba machifu kuwatumikia wananchi wote bila kuzingatia ukoo ama urafiki.
Wakulima hao walisema kuwa machifiu wa lokesheni hiyo wanastahili kutenga siku katika lokesheni hiyo ambayo watu wanakutana na kuwa na mazungumzo ya maendelea kama hapo awali.
“Ni vyema kuweze kutengwa siku moja kila mwezi ya kukutana na kujadiliana masuala ya usalama na maendeleo tuweze kujiinuam,” aliongeza Mokaya Obirim mkazi wa eneo hilo.
Haya yanajili wakati msako wa pombe haramu unaendelea huku baadhi ya wakazi wakiwasuta viongozi ha wa lokesheni kwa kuzembea.
Walikuwa wakiongea katika mkutano wa kikundi cha wakulima wa majani chai ambapo walipewa mafunzo kuhusu jinzi ya kuendeleza kilimo hicho.