Maonyesho ya kilimo ya mwaka 2015 katika Kaunti ya Kisii yanatarajiwa kung'oa nanga siku ya Alhamisi July 9 katika uwanja wa Gusii huku wakulima wakiombwa kuhudhuria ili kupata mbinu mpya za ukulima.
Huku matayarisho yote yakikamili hii leo, baadhi ya wale watakaoshiriki katika maonyesho hayo na waliongea na Mwaandishi huyu Jumatano katika uwanja wa Gusii katika Kaunti ya Kisii walisema kuna mengi ambayo wakulima watapata kusoma kutoka kwa maonyesho ya mwaka huu huku wakiwaomba wakulima wote kufika kwanzia hiyo kesho Alhamisi ili kusoma mbinu mpya za ukulima ambayo wanasema itawafaidi mno.
Miongoni mwa yale wakulima wanatarajiwa kufundishwa nini jinsi ya kutunza mimea katika shamba lao ikiwa wakati wa jua au wakati wa mvua ili kutapa mazao mema kila wakati.
Aidha, wafugaji wa ng’ombe watanufaika kwa kufundishwa jinsi ya kupata aina ya mbegu maalum al maarufu high breed wanayohitaji kama mkulima.
“Tumeandaa mengi ya kuwaelimisha wakaazi wa eneo hili hasa katika sekta ya kilimo kwa hivyo nawaomba wakulima wote kujitokeza kwa wingi kwanzia kesho ili kupata mbinu muhimu za ukulima wao," alihoji mkulima mwandalizi.
Kwingineko, wakazi walikuwa na mengi ya kusema huku wakisubiri maonyesho hayo kuanza rasmi hapo kesho Alhamisi.
Baadhi ya wakazi walisema kuwa kutokana na mbinu walizopata mwaka jana wamesaidika pakubwa haswa katika sekta ya ukulima kwa kuwa mapema mwaka huu kulitokea kiangazi kikubwa, lakini mbinu walizopata ziliwawezesha kupata mavuno bila kushuhudia hasara kubwa.
Mama Cecelia Nyanchoka ni mmoja wa wale waliopata mafunzo hayo mwaka jana na yuko tayari kwa maonyesho ya mwaka huu.
"Kutokana na mafunzo niliyoyapokea ya maonyesho ya kilimo ya mwaka jana, niliweza kupata mavuno mazuri haswa katika ukulima wangu wa nyanya na nipo tayari tena mwaka huu kupata mbinu mpya za ukulima.