Share news tips with us here at Hivisasa

Watu ambao wanatumia eneo la mapumzikoni la Mama Ngina Drive, Likoni katika mji wa Mombasa kupiga picha wageni pamoja na wenyeji wamelalamikia baadhi ya maafisa wa kaunti kuwahangaisha kwa kuwatoza hela ilhali huwa wanalipa pesa kwenye mamlaka husika kila mwezi.

Wapiga picha hao maarufu kwenye eneo hilo la umma wamedai kuitishwa pesa na baadhi ya watu wanaojifanya maafisa wa kaunti, ambapo huwaagiza kutoa kiwango flani ndio wawaruhusu kuendelea na shughuli yao ya kupiga picha ya kila siku ambayo ndio riziki yao.

Wakiongozwa na mmoja wao Ramah Mwakio siku ya Jumapili katika eneo lao la kazi, wafanyabiashara hai walisema kuwa baadhi yao hutegea shughuli hiyo asili mia kwa mia kulisha jamii zao, na si haki hata kidogo kusumbuliwa na kutakiwa kulipa hela ambazo baadhi ya mafisa hao huweka mifukoni na kuzitumia kwenye masuala yao binafsi.

Ramah aliwataka wasimamizi katika idara ya ushuru kwenye kaunti ya Mombasa kuliangazia suala hilo na kuhakikisha kuwa wanawachunguza baadhi ya maafisa hao ambao wamekuwa hata wakiwatishia wanapokosa kutoa hela.

“Wengi wetu vile tuko hapa tuanapiga picha ili kupata hela za kutukimu katika mahitaji yetu ya familia, na hawa maafisa wengine wao wamekuwa wakitutoza hela zisizo za kawaida, kuna wale tunashindwa kulipa ada ya kila siku wakati ambapo hamna biashara na tunaongea na wao kuturuhusu,” alisema Mwakio

Caption:wapiga picha Mama Ngina walalamikia kuitishwa hongo na maafisa wa kaunti ya Mombasa