Share news tips with us here at Hivisasa

Akina mama na vijana katika Kaunti ya Kisii wameshauriwa kujiunga kwa vikundi ili kupata mikopo ambayo itawawezesha kujinufaisha kimaisha.

Akizungumza siku ya Jumapili katika sherehe ya kuchangisha fedha za ujenzi wa kanisa ya kikatholiki ya Nyamagwa, mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Kisii Mary Otara, alisema kuwa akina mama na vijana wanapaswa kujiunga na vikundi ndio waweze kupata mikopo.

“Vijana na akina mama mkijiunga kwa vikundi vya maendeleo mtapata mikopo ambayo itawasaidia katika miradi mbali mbali,” alisema Otara.

Otara alisema kuwa akina mama ndio wana jukumu kubwa la kuinua uchumi wa kaunti kwani wao hufanya kazi ngumu ya kuhakikisha maendeleo yamenawiri katika jamii na kuwaomba viongozi kuwasaidia akina mama ili nao waweze kunufaika na kujiendeleza kimaisha.

“Mimi kama mwakilishi wa wanawake nawaomba akina mama wote na vijana mjiunge katika vikundi mbali mbali ili muweze kujiendeleza kimaisha na kuinua uchumi wa kaunti yetu, kwani sisi ndio tuna jukumu la kuinua viwango vya maendeleo hapa kisii,” alisema Otara.

Otara alisema vikundi vya maendeleo ni muhimu kwa akina mama na vijana kwani ndio nguzo ya kuwasaidia kuinua miradi ambayo wanaanzisha katika maisha yao.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na na wabunge mbalimbali akiwemo mbunge wa Rarieda Nicholas Gumbo, wa Bobasi Steve Manoti wa Mugirango kusini Manson Nyamweya, Omingo Magara na wengine wengi huku wakichangisha zaidi ya Sh3.7m.