Viongozi wameshauriwa kuwa waangalifu wanapozungumza ili kuepuka kuchochea wananchi.
Wito huu umejiri kufuatia matamshi yanayodaiwa kuwa ya uchochezi yaliyotolewa na mbunge wa Gatundu kusini Mosses Kuria siku ya Jumanne.
Akiongea na wanahabari mjini Eldoret mwenyekiti wa baraza la maimam na wahubiri wa dini ya kiislamu katika kaunti ya Uasin Gishu Abubakar Bini alisema sharti mbunge huyo achukuliwe hatua kali ili iwe funzo kwa viongozi walio na tabia kama hiyo.
"Hakunamtu aliye juu ya sheria, mbunge huyo anafaa kushtakiwa," alisema.
Bini alitoa wito kwa wananchi kushirikiana na vitengo vya usalama ili kukabiliana na utovu wa usalama nchini hasa kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani.
Aidha imam huyo alisema kwamba suala la kuhalalisha ushoga na usagaji nchini ni kinyume mila na tamaduni za Kiafrika.