Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kamati ya watu watano imeteuliwa na Kaunti ya Nyamira kuanzisha uchunguzi dhidi ya baadhi ya maafisa waliohusika katika kashfa hiyo.

Haya yanafuatia madai ya matumizi mabaya ya zaidi ya Sh5 milioni na maafisa wa Kaunti ya Nyamira katika mkutano wa ugatuzi uliofanyika katika hoteli moja mjini Kisumu.

Watuhumiwa wa kashfa hiyo wanahusisha baadhi ya maafisa wakuu wa baadhi ya idara, ikiwemo idara ya fedha iliyotwikwa lawama nzito inayoongozwa na John Omanwa, idara ya vijana na utamaduni ikiongozwa na Peter Osoro, idara ya michezo na maafisa na wengineo, ambao wanatarajiwa kuchunguzwa na kamati hiyo teule kuanzia siku ya Ijumaa.

Ikumbukwe kuwa madai ya matumizi na upatilivu wa pesa na maafisa hao ulianza mwishoni mwa mwezi jana ambako uchunguzi ulianzishwa na kubainisha kuwa zaidi ya Sh5 milioni zilitumiwa visivyo, jambo ambalo limezua ghadhabu miongoni mwa umma hata waliotishia kuandamano iwapo suala hilo halitaangaliwa vizuri na kuwashtaki maafisa husika.

Wawakilishi wa wadi katika bunge la Nyamira pia wametaka kuchunguzwa kwa msaidizi wa binafsi wa gavana wa kaunti ya Nyamira Bwana Peter Mochache ambaye inasemekana aliweza kurudisha baadhi ya hela kwenye kaunti hiyo baada ya madai hayo kuzuka.

Mswada huo wa kuwasimamisha maafisa husika kazi kwa muda ili kufanyiwa uchunguzi uliletwa na kiongozi wa wengi katika bunge hilo Bw Raban Masire kwa ushirikiano na Mwakilishi wa Bonyamatuta Beutah Omanga.