Kamati ya akaunti ya umma katika Kaunti ya Nyamira imeanzisha uchunguzi kubaini ni wapi Sh1.1 milioni zilienda baaba ya pesa hizo kujulikana ni wapi zilitumika.
Pesa hizo zinasemekana kuwa baadhi ya maafisa wa kaunti hiyo walipokezwa kufanyia miradi ya maendeleo na kusemekana kuwa huenda zilipotea kwa njia isiyo halali baada ya kubainika kuwa hamna mradi uliofanyika.
Akizungumza na Waandishi wa habari siku ya Jumanne katika mji wa Nyamira baada ya kikao cha wanakamati ya akaunti ya umma katika kaunti hiyo kukamilika ambacho kilindaliwa katika mji wa Kisumu, mwenyekiti wa kamati hiyo Ezra Mochiemo alisema Sh5.5 milioni zilitumika kuwalipa Wawakilisha katika bunge la Kaunti ya Nyamira huku Sh 1.1 milioni hazijulikana ziliko hadi sasa, jambo ambalo liliwapelekea kuanzisha uchunguzi kujua ukweli wa mambo.
Kwa upande wake mkuu wa idara ya fedha katika Kaunti ya Nyamira John Omanwa alisema kufikia sasa tayari Sh385,000 zimepatikana huku zingine zikiendelea kutafutwa ziliko baada ya hizo zilizopatikana kubainika kuwa zililipwa maafisa wa serikali ya kaunti hiyo kupita kiasi kuliko kile kilihitajika kulipwa.
“Tutaendelea na uchungunzi hadi pesa hizo zote zipatikane kwani pesa hizo ni za umma na zinafaa kuwafaidi wakazi wa Kaunti ya Nyamira katika maendeleo,” alisema Mochiemo.
Wakati uo huo, Omanwa aliwataka maafisa wa serikali ya kaunti hiyo kufika mbele ya kamati hiyo ya akaunti ya umma kuelezea jinsi pesa hizo zilipotea na kueleza kwa nini pesa hizo hazikurudishwa wakati hazikutumika ili uwazi uonekane kwa wananchi wa kaunti hiyo.