Serikali ya Kaunti ya Kisii kupitia sekta ya afya imeombwa kununua dawa za kukabiliana na funza katika kaunti hiyo.
Akiongea hii leo Jumatano katika maeneo ya Menyikwa Wadi ya Kisii ya Kati, eneo Bunge la Nyaribari Chache katika Kaunti ya Kisiiwakati alitembelea familia moja ambayo watoto wao watatu wa miaka 14, 25 na 16 wameathiriwa na funza, mhudumu wa afya ya jamii katika kaunti hiyo Kepha King’oina alisema kuwa bado funza ni changamoto kubwa kwa baadhi ya Jamii katika mji wa Kisii ambao wanataka kusaidiwa na sekta ya afya ya Kaunti ya Kisii.
"Naiomba Serikali yetu ya Kaunti ya Kisii kupitia sekta ya afya kukubali kuwa bado kuna changamoto ya funza katika jamii na kutoa madawa ya kuwasaidia waathiriwa hao,” alihoji King’oina.
King’oina alisema kuwa baadhi ya wasimamizi wa afya katika Kaunti ya Kisii hawataki kusikia na kukubali kama kuna changamoto ya funza katika eneo hilo, jambo ambalo amewaomba wasimamizi hao kukubali na kutoa huduma ya afya kwa waathiriwa ili kuepuka na janga hilo katika jamii zao.
Kwingineko, King’oina alisema kuwa umaskini ndio huchangia funza hao katika jamii kwani katika familia ya watoto hao watatu alipotembelea siku ya Jumatano ambao ni mayatima hawana mbele wala nyuma, hali ambayo alisema kuwa imewaachabila kuwa na uwezo wa kutafuta dawa za kumaliza funza hao ambao King'oina amesema kuwa wamekuwa kero kubwa kwa maisha ya wengi katika eneo hilo.
Kwa sasa King'oina ameomba familia zingine kutouza shamba akidai kwamba kitendo hicho ndicho husababisha ufukara kwani ufukara utawapelekea kuishi kwa maisha yasiofaa na kutowawezesha kupambana na maradhi mbali mbali.