Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wakaazi wa eneo la Gusii wamewataka ma gavana wa Kaunti ya Kisii na Nyamira kuhakikisha usalama upo katika kaunti hizo mbili.

Wito huu umewadia baada ya usalama kudorora haswa mpakani Keroka iliyoko katikakati mwa Kaunti ya Kisii na ya Nyamira. Gavana James Ongwae wa Kisii na Gavana wa Nyamira John Nyagarama wameombwa kuungana kuimarisha usalama katika mji huo.

Keroka inasemekana kuwa ipo katika mpaka wa kaunti hizo mbili, jambo ambalo linakuwa kikwazo kwa serikali hizo mbili kushindwa ni serikali ipi inastahili kuimarisha usalama katika eneo hilo na kupelekea wakazi hao kuwasihi viongozi hao kuungana, kushirikiana pamoja kuimarisha usalama katika eneo hilo.

Visa vya uhalifu na ujambazi vimekuwa vikishuhudiwa katika eneo hilo la Keroka kila wakati kufuatia kudorora kwa usalama.

Wakizungumza na Waandishi wa habari siku ya Jumatatu katika mji wa Keroka, wakazi wa eneo hilo wakiongozwa na George Morara waliomba viongozi hao kuimarishwa usalama katika eneo hilo ikiwa wanahitaji kukomesha uhalifu katika eneo hilo na kupunguza visa vya wakazi wa eneo hilo kushambuliwa kila mara.

“Tunaomba Magavana wa Kisii na wa Nyamira James Ongwae na John Nyagarama kuweka kando masuala ya kujiuliza ni serikali ipi inastahili kuweka usalama katika eneo hilo la Keroka na kushirikiana kuweka usalama eneo hilo kwani hao wana uwezo wa kuiomba serikali kuu kuwatuma maafisa wa polisi wa kutosha kuimarisha usalama katika eneo hili,” alisema Samuel Omwanza, mkazi.

Ni wiki moja tu baada ya mwanamume mmoja kuawa katika eneo la Keroka.