Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mbunge wa Bomachoge Chache, Kaunti ya Kisii Simon Ogari amewaomba waendeshaji bodaboda kutotumiwa na wanasiasa kuwatusi baadhi ya viongozi.

Akiongea siku ya Jumatatu katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Tendere iliyoko eneo bunge lake alipokutana na waliohudhuria kikao cha bunge mashinani, iliyobuniwa kukusanya maoni ya wakazi wa eneo bunge hilo kuyahusu miradi kupitia hazina ya ustawi ya maeneo bunge (CDF), mbunge Ogari aliwaomba wahudumu hao wa bodaboda kuyazingatia mambo yatakayowasaidia siku zijazo.

“Nawomba vijana katika eneo bunge hili kutokubali kutumiwa na wanasiasa wanao nia moja tu ya kujifaidi wao wenyewe maanake shida ikitokea, kwa mfanu mkipelekwa kortini au katika jela kwa makosa hayo, ndio mtajua viongozi hao hawatawasaidia kamwe,” alisema Mbunge Ogari, wa Bomachoge Chache.

“Wale wanaojua siasa yangu watawahakikishia kuwa sijawahi patia mtu hata mmoja pesa ili aende kumtusi mtu fulani kwa sababu siasa ya aina hiyo sio ya maendeleo. Nawaomba wahudumu wa bodaboda na vijana kwa jumla kuwaheshimu viongozi walioko mamlakani,” aliongeza Ogari.

Aidha, aliwataka wanasiasa kukoma siasa za aina hiyo za kukabidhi baadhi ya vijana pesa kwa nia ya kuwatusi baadhi ya viongozi huku akisema heshima ndio inahitajika katika kila jamii.

“Nawomba wale wanasiasa kutumia pesa wanaowapatia vijana kusababisha rabsha na kuleta chuki katika kufanya maendeleo ili sisi kama viongozi tusaidie kubadilishe maisha ya wananchi,” alidokeza Ogari.

Matamshi hayo yaliunga mkono na watu walikuwa katika bunge mashinani hilo huku wengi wakisema siasa mbaya huleta maisha mbaya ambayo yasio bora katika jamii.