Polisi mjini Molo wanamzuilia mwanaume mwenye umri wa miaka 19 kwa tuhuma za kushiriki ngono na kondoo.
Mwanamume huyo anayefanya kazi katika hoteli moja mjini Molo alifumaniwa akila uroda na kondoo huyo ndani ya shamba moja la mahindi kabla ya majirani kuitwa na kumpatiliza kichapo cha mbwa.
Bi Lucy Njeri ambaye ni Mkulima wa mifugo mjini Molo alielezea jinsi alivyopata mwanamume huyo akitekeleza uovu huo kabla ya kuwapasha habari majirani ambao walimnasa mwanamume huyo aliyejawa na hofu asiweze kuhepa wala kuvaa suruali ili kujinasua kutoka eneo la tukio.
Maafisa wa usalama waliokuwa katika shughuli za kumwaga pombe haramu walifika katika eneo la tukio hilo na kumuokoa jamaa huyo aliyekiri kutekeleza kosa hilo.
Wakazi wa kijiji cha Tayari mjini Molo walionyesha masikitiko yao kuhusiana na kisa hicho huku wakitaka hatua kuchukuliwa dhidi ya jamaa huyo.
“Kitendo cha kumchafua mnyama kimelaaniwa hata kwenye kitabu takatifu. Pia ni kinyume na maadili pamoja na tamaduni za kijamii kwa mtu kufanya mapenzi na mnyama. Kama wakazi wa Molo tumesikitika sana, " alisema Charles Njenga, mkazi Molo.
Njenga amewataka vijana kueleza waziwazi maswala ambayo yanawakabili badala ya kuishi maisha ya kujitia hamnazo na baadaye kufanya vitendo vya unyama na uvujaji wa sheria.
“Siwezi kuelezea ni matatizo yapi yamewapata vijana hasa hapa kwetu Molo kwa sababu visa vya uhalifu vimeongezeka na kufikia viwango vya kuogofya. Hivi majuzi watoto walikuwa wananajisiwa kisha kuuwawa," alisema Njenga.
Njenga aliliongezea kuwa: "Hata wakongwe walikuwa wanadhulumiwa. Sijui kama ni unyama umewatoka wanyama na ukaingia binadamu. Kitendo hiki kinatutia aibu sana sisi wanaume."
OCS wa Kituo cha Polisi cha Molo Bw John Manyara alisema mshukiwa atafikishwa mahakamani pindi tu uchunguzi utakamilika.