Gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwae amewaomba viongozi kushirikiana kuleta maendeleo katika kaunti ya Kisii.
Ongwae amewakaribisha wabunge, wawakilishi wa wadi, mwakilishi wa wanawake na seneta kujiunga pamoja kuwaletea wananchi wa kaunti hiyo maendeleo kikamilifu kabla ya mwaka wa 2017.
Akiongea siku ya Jumapili mjini Marani, Ongwae alisema bila ushirikiano kati ya viongozi waliochaguliwa, maendeleo hayatashuhudiwa kamwe katika kaunti hiyo.
Alisema kuwa viongozi kujitenga kushirikiana kwa maendeleo ni jambo ambalo si la kufurahisha.
Gavana Ongwae alisema ameweka mikakati ya kuyatimiza yale yote ambayo aliahidi wananchi wa kaunti hiyo wakati wa kampeini.
“Naomba tuweke siasa kando maana tumekuwa kwa ofisi kwa miaka miwili na nusu pekee na hatujatimiza yale yote tulisema. Tunajaribu kutimiza ahadi zutu na ninaamini kuwa tutafanya yote kabla ya 2017,” alisema Ongwae.
Aliongezea, “Naomba ushirikiano wa viongozi wote, tuwe tunafanya maendeleo pamoja.”
Wakazi nao walifurahishwa na Gavana Ongwae kukaribisha viongozi wote kushirikiana kuletaa maendeleo huku wakisema bila ushirikiano hakuna maendeleo yatafanywa katika kauunti ya Kisii.
“Nasi kama wananchi tutaona vizuri viongozi wakishirikiana pamoja kwani lile tunahitaji ni maendeleo kutoka kwa viongozi wetu,” alisema John Onsarigo, mkazi.