Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wafanyibiashara wa soko ya Marani iliyoko eneo bunge la Kitutu chache kaskazini wamemuomba gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwae kuharakisha ujenzi wa soko alioanzisha mwaka jana.

Wito huo umetolewa baada ya wafanyibiashara hao kusema wanasumbuka kwa kunyeshewa kwa kutokuwa na vibanda vya soko.

Wafanyibiashara hao walisema wanaendelea kupata hasara kubwa haswa wakati mvua inaponyesha kwani wao hulazimika kuondoa bidhaa zao.

Wakizungumza na mwandishi huyu siku ya Jumanne katika soko hiyo ya Marani, wafanyibiashara hao wakiongozwa na Mary Mose waliomba ujenzi huo kuharakishwa na kusema kuwa wanasumbuka ilhali wanaendelea kutozwa ushuru bila kufanyiwa maendeleo.

“Ujenzi huu ulianzishwa na ukasimama kwa muda lakini hatujui ni nini kinafanya ujenzi huu kusimamishwa. Tunajua serikali ina pesa nyingi kwani tuanlipa ushuru. Kile tunaomba gavana wetu atufanyie ni kumaliza ujenzi wa soko hili,” alisema Jane Bosibori, mfanyibiashara.

Aidha, wafanyibiashara hao waliomba kujengewa vyoo vya kisasa katika soko hilo huku wakisema kuwa vyoo ambavyo viko katika soko hilo vimeharibika.

Walisema kuwa wanahitaji kujengewa vyoo vingine ili waweze kuimarisha katika soko hilo.

“Vyoo ambavyo tunatumia si vya kuridhisha kwani vimeharibika. kama gavana anatujali kama watozwa ushuru, tunaomba ajenge vyoo vipya na kumaliza ujenzi wa soko,” alisema Peter Ombae, mfanyibiashara.