Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wakazi wa mji wa Kisii wameipongeza serikali ya kaunti ya Kisii kwa kutenga shamba litakalo tumika kwa ujenzi wa kituo cha mapumziko karibu na kituo cha magari kama njia moja ya kuwasaidia na mahali pa kupumzika.

Wakiongea na mwaadishi huyu siku ya Jumapili katika mji wa Kisii baadhi ya wakazi walipongeza serikali ya kaunti kwa kutenga shamba ambalo kituo hicho kitajengwa huku wakiiomba serikali hiyo kuharakisha na kujenga kituo hicho ili kuwasaidia wakazi hao na mahali pa kupumzikia.

Wakazi hao walilalamika kuwa mara nyingi serikali ya kaunti hutenga shamba litakalotumika kwa miradi mbalimbali lakini baadaye hupata shamba hizo zimenyakuliwa na watu binafsi jambo ambalo huwakera na kuomba seriklai ya kaunti kuhakikisha imejenga kituo hicho.

Wakazi hao waliongezea kuwa kuwepo wa kituo hicho ni njia moja ya kaunti ya Kisii kuendelea katika sekta ya kitalii na uchukuzi kwani watu wataweza kuja na kupumzikia hapo wakitafuta mahali pa kufanya biashara na wengine wakingojea kusafiri.

“Napongeza serikali ya kaunti yetu ya Kisii kwa kutoa shamba hili kwa kutujengea kituo cha mapumziko, ”alisema Edward Nyang’au mkazi.

Aidha, wakazi hao waliwakashifu wanaonyakuwa mashamba ya uma katika mji wa Kisii huku wakisema kuwa hao ni wale wanaojitakia makuu bila kuwajali wengine na kuiomba serikali ya kaunti kuwachukulia hatua ya kisheria wanyakuzi hao.

“Naomba walio na tabia ya kunyakuwa mashamba ya uma ambayo serikali ya kaunti imetenga kwa ajili ya kuazisha miradi mbalimbali kujali wengine kwani shamba hilo ni la kusaidia watu wote,” alisema William Antambo, mkazi.