Share news tips with us here at Hivisasa

Mkuu wa Idara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo katika Kaunti ya Kisii Moses Onderi amewahakikishia wakazi wote wa kaunti hiyo kuwa stakabadhi zote za ardhi zipo salama salami katika ofisi yake.

Hii ni baada ya ofisi hiyo kuvunjwa na wezi wasiojulikana mnamo siku ya Jumapili usiku na kuiba bidhaa mbalimbali za kaunti hiyo.

Akizungumza siku ya Jumatatu na Waandishi wa habari katika ofisi yake iliyoko mjini Kisii, Onderi alikiri kuwa watu wasiwe na wasiwasi kuwa stakabadhi zao za ardhi zilipotea na kuwahakikishia kuwa stakabadhi ziko vizuri na kusema huenda ofisi hiyo ikafungwa kwa muda ili baadhi ya bidhaa vipangwe tena uchunguzi unapoendelea kubaini ni akina nani waliotekeleza wizi wa aina hiyo.

“Mahala stakabadhi za shamba zilikuwa haikufikiwa na wezi hao, lakini uchungunzi umeanzishwa na maafisa wa polisi kujua waliotekeleza wizi huo ili waweze kutiwa mbaroni na kuchukuliwa hatua kali ya kisheria,” alisema Onderi.

Ni mwezi mmoja tu umepita tangu stakabadhi za ardi katika Kaunti ya Kisii kupangwa kwa njia ya kidigitali baada ya kuagizwa na waziri wa muda katika Wizara ya Ardhi nchini Fred Matiang’i.

Kitendo cha kuvunjwa kwa maofisi ya serikali katika Kaunti ya Kisii kimekuwa kikitekelezwa kila mara huku wakati wa maonyesho ya kilimo yaliokamilika mwezi Juni terehe 12 mwaka huu, ofisi ya mkurugenzi wa kilimo katika kaunti hiyo ilivunjwa na mali kuporwa hasa tarakilishi na baadhi ya bidhaa vingine.

Pia ofisi za NEMA nazo zilivunjwa na bidhaa mbalimbali kuchukuliwa, lakini kwa sasa uchunguzi unaendelea kubaini wale wanaotekeleza wizi wa aina hiyo katika ofisi za serikali za Kaunti ya Kisii.