Wahudumu wa bodaboda katika eneo la Kinoo wamepewa onyo kali dhidi ya kushirikiana na majambazi.
Wale watakaopatikana watatimuliwa katika chama cha waendeshaji bodaboda na kurepotiwa kwa polisi.
Hii ni baada ya mhudumu mmoja kujipata mashakani aliposhikwa na maafisa wa polisi akiwa na mshukiwa wa ujambazi ambaye amekuwa akisakwa kwa muda wa miezi sita kufuatia uovu ambao ametekeleza.
Mhudumu huyo alishikwa kwa madai kuwa yeye ndiye humsafirisha wakati anapoenda katika shughuli zake za ujambazi na kisha kumtorosha kunapoenda visivyo.
Akizungumza katika mkutano wa dharura wa waendeshaji bodaboda katika eneo hilo siku ya Ijumaa, mwenyekiti wa chama cha waendeshaji bodaboda eneo la Kinoo Francis Wambugu alisema alisikitika kuskia kisa cha mmoja wao ambao alikuwa anashirikiana na majambazi kushikwa na maafisa wa usalama.
Alisema mhudumu huyo anaweza leta maafa makubwa katika biashara yao, na kuongezea kuwa mambo kama hayo halifai kuwa miongoni mwao kwa kuwa lengo lao ni kuwasaidia wananchi hasusan wakati wa usiku bali is kushirikiana na majambazi.
Alisema yeyote atakayeshukiwa kufanya hivo atatimuliwa katika chama chao na kurepotiwa kwa maafisa wa usalama.
Alisema jambo hilo limezua maswali kiasi ambacho wakubwa wanapanga mikakati kuhakikisha kuna masaa ambayo wahudumu wanafaa kuwa wamefunga kazi.
"Hatutakubali kufanya kazi na wahalifu miongoni mwetu. Yeyote atakayepatikana tutamtimua kisha kumfikisha kwa maafisa wa usalama," alisema Bwana Wambugu.
Alisema chama cha waendeshaji bodaboda kinafanya kazi kwa karibu na maafisa wa usalama kuhakikisha jambo hili limekomeshwa.