Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wafanyibiashara katika soko la Daraja Mbili ilioko mji wa Kisii wameiomba Serikali ya Kaunti ya Kisii kuwajengea kivukio cha juu ili kupunguza ajali za barabara katika eneo hilo.

Hii ni baada ya watu wengi kugongwa na magari yanayoleta msongamano mkubwa katika barabara inayopita katikati mwa soko hilo kila kuchao.

Wakizungumza na Mwandishi huyu leo Alhamisi katika soko hilo, wafanyibiashara hao wakiongozwa na Teresa Kerubo Omae walisema kuwa watu wengi hujeruhiwa kwa kupitia ajali ya barabara yanayoendeshwa kwenye eneo hilo, jambo ambalo limewalazimu kuomba Seriklali ya Kaunti kuingilia kati na kuwajengea kivukio.

"Juma lililopita gari lilinigonga hapa lakini uzuri gari hilo halikuwa linaendeshwa katika mwendo wa kasi. Naiomba serikali isikie kilio chetu ili maisha yetu yasiwe hatarini kila tunapovuka barabara hili,” alihoji Lydiah Bosire muuza nyanya katika soko hilo la Daraja.

"Kwa upande wangu huwa ikifika siku ya soko kama leo Alhamisi siku ya soko katika soko hili la Darajani Mungu tu ndiye hua tunamwomba ili atufikishe mwisho wa siku maana ni rahisi sana mtu kugongwa na gari wakati wowote kabla ya kurudi nyumbani,” alidokeza Jastus Osinyo mfanyibiashara wa kuuza begi katika soko hilo.

Ni jukumu la Serikali ya kaunti kuingilia kati ombi la wafanyibiashara hao ili kuwasaidia kuepuka na uwezekano wa ajali kwenye eneo hilo.

"Tukijengewa kivukio hicho tutafurahi sana maana itakuwa rahisi kwetu kuvuka kuelekea ng’ambo ile na tutafanya ubadilishanaji wetu bila taswishi yoyote," aliongeza Osinyo.