Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakazi wa Matutu, Wadi ya Gesima walio karibu na mtambo wa umeme wameiomba kampuni ya nguvu za umume kuwajibika na kurekebisha nyaya ambazo zinaninginia kutoka kwa mtambo huo.

Wakiongea siku ya Jumatano katika eneo la Matutu, baadhi ya wakazi hao waliiomba kampuni ya nguvu za umeme kufika katika eneo hilo na kurekebisha nyaya hizo ambazo zimeleta hofu kwao.

Wakazi hao walisema kuwa mtambo huo ambao umewekwa karibu na shule ya upili ya Matutu unastahili kushughulikiwa kila wakati ili usije ukaleta shida katika kijiji hicho.

Kwa sasa wameiomba wanaoshughulikia masuala ya nguvu za umeme kufika mahali hapo na kutengeneza nyaya hizo huku wakiwaomba wawe wakiziunganisha kwa njia ya kudumu.

“Naomba wanaosimamia masuala haya ya nguvu za umeme kutusaidia ili tusiwe na uoga wa kuwa karibu na mitambo hii,” alisema  Japhet Okioga, mkaazi.

Aidha, waliwaomba wenzao kukata miti iliyoko karibu na nyaya za stima huku wakisema mti hiyo inaweza leta shida haswa kwa watoto wa eneo hilo wanaokwea miti kwa ajili ya kutafuta kuni.

"Tunaomba wenzetu ambao wamepanda miti karibu na nyaya za stima wawe wanakata mti hiyo ili isije ikaleta shida katika kijiji hiki,” alisema Samwuel Kiage, mkazi.

Kwigineko, wameiomba serikali ya kaunti hiyo kushirikiana na kampuni hiyo kuwasaidia wakazi wengine kupata stima hasa wakati huu ambapo gharama yake imeshuka.

Mtambo wa stima. Wakazi wa Matutu wameomba kampuni ya nguvu za umemu kuwajibika na kurekebisha nyaya ambazo zimening'inia kutoka mtambo huo.